Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria katika hafla ya awali. [Picha/ standardmedia.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria anataka maafisa wa Tume ya IEBC ambao hawakutia sahihi fomu 34B katika maeneo bunge matatu Kaunti ya Mombasa kuchukuliwa hatua.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za chama cha Jubilee jijini Mombasa, Kuria alisema kuwa maafisa hao walikiuka katiba na wanastahili kushtakiwa.“Maafisa hao walivunja sheria za uchaguzi wa taifa na sharti washtakiwe mahakamani,” alisema Kuria.Kuria anataka maafisa waliosimamia uchaguzi katika eneo bunge la Nyali, Likoni na Kisauni kukabiliwa na mkono wa sheria ili kuwa funzo kwa wengine.“Maafisa hao wanapaswa kutiwa mbaroni ili iwe funzo kwa wengine siku za usoni,” alisema Kuria.Vile vile, amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuwa makini ili kuhakikisha makosa kama hayo hayatokei tena.Aidha, Kuria amemtaka kinara wa NASA Raila Odinga kukubali tarehe ya uchaguzi ili kuepuka kuwa na hali ya taharuki nchini.Mbunge huyo alisema kuwa huenda joto la kisiasa likaathiri sekta ya utalii iwapo wanasiasa watazidi kuwagawanya Wakenya.