Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huenda shughuli za upanuzi wa barabara kuu Mombasa zikakosa kutekelezwa kutokana na mzozo wa maswala ya umiliki wa ardhi kushindwa kutatuliwa.

Kulingana na katibu katika Wizara ya Uchukuzi na miundo msingi nchini John Mosonik, shughuli hiyo haiwezi kuendelea jinsi ilivyoratibiwa iwapo maswala ya umiliki wa ardhi utazidi kulemaza shughuli za upanuzi wa barabara.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa baada ya kutembea baadhi ya barabara ambazo zimeidhinishwa kufanyiwa ukarabati katika kaunti hiyo, Mosonik alisema kwamba serikali ya kaunti ya Mombasa inafaa kuchukua jukumu la kuwatafutia ardhi wakaazi wanaoishi katika ardhi za serikali ili kupunguza mzigo kwa serikali ya kitaifa.

“Serikali ya kaunti ya Mombasa inafaa kuingilia kati swala hili na kuwatafutia makao wakaazi wanaoishi katika ardhi za serikali badala ya wao kuzozona kila uchao.Iwapo swala hilo basi litatatuliwa kwa haraka shughuliza upanuzi wa barabara hazitakuwa na pingamizi,” alisema Mosonik.

Mosonik amesema kwamba shughuli hiyo inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwaka mmoja ili kupunguza msingomano wa magari ya uchukuzi wa mizigo na ule wa umma katika barabara kuu za kaunti ya Mombasa na ile ya kuelekea jijini Nairobi.

“Upanuzi wa barabara kuu katika kaunti ya Mombasa zitapunguza kwa kiasi kikubwa msongamono wa magari ya uchukuzi,ikiwa barabara zetu ni pana. Sasa ni jukumu la serikali ya kaunti kusaidiana na seriokali kuu ili kutatua mzozo wa umiliki wa ardhi na tumalizane nah ii shughuli,” aliongeza Mosonik.

Wanakandarasi wa kujenga barabara hizo wamelalamikia kuhangaishwa na baadhi ya viongozi wa kaunti pamoja na wakazi wanaodai kufidia kabla ya kuhama maeneo yaliyotengwa kujengwa barabara hizo.