Wafanya kazi pamoja na maafisa wa Hospitali Kuu ya Kisii Level six walifaulu kuuzima moto uliozuka kwenye afisi ya wauguzi katika hospitali hiyo mjini Kisii mchana wa leo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akijibu maswali ya wanahabari kuhusu kisa hicho, Mkuu wa Wauguzi Merlene Makone alieleza kuwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa walihamishwa kutoka eneo la hatari la Wodi Nambari Sita, ambako moto ulizukia, punde tu ulipoonekana.

Aliwafamisha wanahabari kwamba chanzo cha moto huo ulioteketeza viti meza na bidhhaa ndogo binafsi za wauguzi zilizokuwa zimehaifadhiwa afisini, ni hitilafu ya nguvu za umeme, iliopelekea moto huo kuwaka na  kusababisha uharibifu huo.

“Hamna haja ya hofu wala wasiwasi, kila kitu kiko sawa," alisema, huku akikanusha baadhi ya madai na ripoti ambazo zimesambazwa kwamba moto huo ulharibu mali yenye thamani kubwa na kuharibu jengo la wodi hiyo liitwalo Wodi la Nyangito.

Aliongeza kusema kwamba wafanyakazi wa hospitali hiyo walifanikiwa kuuzima moto huo kwa kutumia maji, mda mfupi baada ya kugundua moshi ukichomoka kutoka afisi ya wauguzi iliyopakana na Wodi ya Nyangito.

Hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo la za saa saba na nusu alasiri.

Kwa sasa, shuguli za matibabu katika hospitali hiyo zimerejea na zinaenedelea kama kawaida.