Zaida ya wanafunzi 2,000 wa darasa la kwanza na pili jimbo la Nakuru watanufaika na elimu ya dijitali iliyoanzishwa na serikali katika shule ya msingi ya St. Marys Girls, mashariki mwa Nakuru.
Mpango huu pia utahusisha shule ya msingi ya Keringet.
"Mfumo kama huu utaanzishwa katika shule nne za msingi ambazo ni za wanafunzi vipofu ili kuleta usawa katika elimu," alisema mkurugenzi wa elimu wa Nakuru Esther Muiru.
Kulingana na meneja wa utekelezaji wa chuo kikuu cha JKUAT, Shadrak Mutilangi, alisema kwamba vifaa 120 vya dijitali vimewekwa katika shule za msingi kulingana na idadi ya wanafunzi.
"Vifaa hivi vimepimwa na vinaweza kutumika kwa urahisi kati ya walimu na wafunzi," alisema.
Chuo kikuu cha JKUAT kitashiriki katika kupeleka vipatakilishi katika majimbo 21.