Mradi wa hivi punde wa Mwakilishi wa wadi ya Gachuba, Andrew Magangi, wa kupanua baadhi ya barabara katika eneo lake umetia kasi sasa baada ya mashine husika za kuonekana katika eneo hilo zikipanua na kukarabati baadhi ya barabara.
Magangi, ambaye amekuwa akionekana akikagua ukarabati huo, amewasihi wenyeji kukubali zoezi hilo liendelee ingawa litachukulia kama linaloharibu mazingira.
Akiongea katika mazishi ya Edward Makori katika kijiji cha Keboba, Magangi pia aliwaomba wenyeji msamaha kwa kuchelewa kufanya zoezi hilo ambalo lilikuwa ni ahadi yake katika kampeni za mwaka 2013.
Magangi, ambaye pia ni msaidizi wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Nyamira, amewahidi wanainchi kutarajia mengi mazuri kabla na baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya barabara zilizokarabatiwa na kupanuliwa ni za Gachuba-Nyariacho, Gachuba-Miriri, Keboba-Bochorike, Girango-Kenani-Gachuba na zinginezo.
Wenyeji sasa wanaiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kudhibiti mkondo wa maji na mchanga katika barabara hizo zilizokarabatiwa.