Serikali kuu sasa imeanza awamu yake ya kwanza ya mradi wa kusambaza vipatakilishi kwa wanafunzi wa shule za umma nchini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mradi huo umezindiliwa rasmi mjini Mombasa katika Shule ya Msingi ya Spaki huku wanafunzi na walimu wakikabidhiwa vipatakilishi hivyo kutoka Wizara ya Elimu na Teknolojia nchini.

Mwalimu mkuu wa Shule ya Sparki mjini Mombasa Alfred Nthiga amesema kuwa amefurahia hatua hiyo ya serikali huku akisema kuwa itaboresha zaidi viwango vya elimu nchini.

Aidha, ameishinikiza serikali kuipa swala la elimu kipau mbele hasa kwa kutenga fedha zaidi ili kuwawezesha walimu kutekeleza majukumu yao vyema kutokana na kuwepo vya vifaa vya elimu vya kutosha.

"Tunashukuru serikali kuu kwa kutuletea vipatakilishi kwa Shule yetu ya Spaki. Pia tunaiomba serikali kuhakikisha kuwa swala la elimu linapewa kipaumbele,” alisema Nthiga.

Vipatakilishi hivyo vimekuja vikiwa na silabasi ya masomo ya hisabati, kiingereza, sayansi na kiswahili.

Hata hivyo, mradi huo wa serikali ya Jubilee unatarajiwa kusambazwa kote nchini ili kuwanufaisha wanafunzi wa shule za msingi za umma.