Gavana wa kaunti ya Taita Taveta John Mruttu ameshtumu hatua ya kupunguziwa idadi ya walinzi magavana hasa Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho sawa na kumpukonya liseni ya kumiliki silaha.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mruttu amesema kuwa hatua hiyo ya serikali kuu yaonyesha kudorora kwa Uhuru wa kidemokrasia nchini huku akisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwaadhibu wakosoaji wa serikali badala ya kushughulikia uhaba wa maafisa wa polisi nchini.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumanne, Mruttu amesema kuwa Joho hajawahi kutumia visivyo bunduki yake ama kutishia yeyote wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa hivi majuzi mjini Malindi, hatua kama hiyo ikichukuliwa dhidi yake.

"Serikali inafanya makosa makubwa sana kuwapokonya walinzi na silaha magavana, hatua hiyo inalenga kuwanyanyasa na kuwaweka viongozi hao katika hali ya hatari, lazima serikali kuangalia swala hilo vyema na kuwapa ulinzi viongozi hao," alisema Mruttu.

Kiongozi huyo ameitaka serikali kuhakikisha kuwa magavana na viongozi wengine wanaopewa ulinzi ili kuzuia viongozi hao kuandamwa na mahasidi wao.