Sekta ya uchukuzi ilisimama kwa mda katika barabara ya Kisii-Nyamira baada ya maafisa wa usalama kuzuru eneo hilo kwa shughli ya msako.

Share news tips with us here at Hivisasa

Madeva watatu walitiwa mbaroni na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Nyamira wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Akitibithisha hayo mkuu wa polisi katika kaunti ya Nyamira Ricah Ongare alisema zoezi hilo liliendeshwa ili kuhakikisha sheria za barabarani zinafuata bila kuvunjwa.

Aidha, magari sita yalikamatwa kwa kutozitimiza sheria za barabarani huku ikibainika kuwa magari mengi ufanya biashara ya uchukuzi bila kufuata sheria za barabarani.

Zoezi hilo lilipelekea magari mengi kufichwa na wenyeji wao kwa hofu ya kukamatwa .

“Kuna dareva mmoja ambaye alikuwa na makosa na akatoroka lakini tumemfuata na tayari tumempeleka katika kituo cha polisi,” alisema Ongare.

Zoezi hilo lilipongezwa na wasafiri ambao walisema baadhi ya madereva hubugia pombe na kuendesha magari katika hali inayohatarisha maisha yao.