Mshauri wa kifedha wa benki ya dunia tawi la Kenya Charles Mochama amejitokeza kuwasihi wakazi wa kaunti ya Nyamira kuwakubali watu waliokuwa wafungwa kwenye jela katika jamii.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye mahojiano siku ya Jumatatu, Mochama alisema kuwa yafaa jamii iwakubali wafungwa wanaosamehewa na serikali ili kurejea katika jamii.

"Ni ombi langu kwa wakazi wa kaunti ya Nyamira kuwakubali wafungwa wanaosamehewa na serikali ili kujiunga na wananchi kwenye jamii kwa maana wao ni ndugu zetu," alisema Mochama. 

Mochama aidha aliwasihi wananchi kutowabagua wafungwa katika jamii akihoji kuwa wengi wa wafungwa hubadili tabia zao baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao kwenye jela. 

"Nawaomba wananchi kutowabagua wafungwa kwa maana idadi kubwa ya wafungwa hubadilisha tabia zao pindi baada yakumaliza vifungo vyao," aliongezea Mochama.

Picha: Mshauri wa kifedha wa benki ya dunia tawi la Kenya Charles Mochama. Amewataka wananchi kukubali watu ambao wana historia ya uhalifu na ambao wametumikia vifungo gerezani. WMaina/Hivisasa.com