Kinyozi mmoja katika kata ya Mbaruk, kaunti ndogo ya Gilgil ameenda mafichoni baada ya kuwadhulumu kimapenzi vijana wapatao kumi.
Akidhibitisha tukio hilo siku ya Ijumaa, afisa tawala wa kata ya Mbaruk, Humphrey Mwangi alisema wameanzisha msako kumtafuta mushukiwa kwa minajili ya kumtia mbaroni na kumpeleka kortini afunguliwe mashtaka.
Mshukiwa, Peter Kariuki aliye na miaka 26 ameshutumiwa kwa kuwanyanyasa kimapenzi vijana wadogo wenye miaka tisa na kumi na tatu .
Akisimulia masaibu yaliompata mwanae, Mary Muthoni alisema kwamba aligundua masaibu mwanae alikua anapitia baada ya kuona kuwa ameshindwa kutembea kama kawaida.
“Kariuki alimhadaa na peremede, akamuingiza katika nyumba yake, akamfunga mikono na mdomo ,kisha akamudhulu,” akasema Muthoni,ambaye mwanae mwenye miaka 10 ni mwaadhiriwa.
“Alikuwa akitembea mguu moja juu na mwingine chini,” alizidi kuongea Muthoni.
“Kariuki alinipa peremede, akaniahadhaa tuandamane naye kwake, akanifungia ndani ya nyumba na kunifunga mikono ,halafu akanitedea 'uchafu'’ alisema mototo mmoja.
Wakaazi wa Mbaruk wametoa wito kwa serikali kuimarisha usalama wa watoto wao, hasa wakati huu wa likizo ndefu ya Desemba na kuwachukulia hatua kali washukiwa wa dhuluma za kimapenzi dhidi ya watoto wao.
Afisa tawala Mwangi alisema jitihada zimeimarishwa za kumtafuta mushukiwa na atepelekwa mahakamani punde watakapo mtia mbaroni.