Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini na saba alifikishwa mbele ya mahakama moja ya Kisumu kujibu mashtaka ya wizi wa mabavu.

Malcom Okome alikana makosa hayo mbele ya hakimu mkuu wa Kisumu Thomas Obutu siku ya Jumanne.

Okome anadaiwa kutekelekeza kosa hilo tarehe ishirini na nne mwezi jana mjini Kisumu.

Mahakama ilielezwa kuwa, mshatakiwa alimvamia Janet Akinyi nyumbani kwake mtaani Manyatta usiki wa tarehere ishirini na nne.

Wakati wa uvamizi huo, Akinyi alikua nyumbani kwake pekee yake na Okome anadaiwa kuvuka uua linalozingira nyumba ya mlalamishishi na kuvunja mlango.

Okome alidaiwa kumjeruhi Akinyi kwa kumpiga alipokataa kumpea pesa alizokuwa akiitisha.

Ilisemekana kuwa Okome hatimaye aliiba shilingi elfu kumi na simu ya rununu.

Baada ya uvamizi, Akinyi alipiga kamsa zilizowavutia majirani waliokuja kumsaidia na kumpeleka hospitalini. Alilazwa hospitalini kwa mda wa siku mbili kutokana na majeraha aliyoyapata.

Polisi waliarifiwa kuhusu uvamizi huo na uchunguzi ukaanzishwa mara moja. Walifanikiwa kumnasa Okome baada ya kutafuka simu iliyoibiwa.

Hakimu Obutu alimwachilia mshtakiwa kwa thamana ya shilingi elfu kumi, huku kesi ikitazamiwa kuanza tarehe ishirini na tisa mwezi ujao.