Mshukiwa aliyekamatwa na bunduki inayodaiwa kuibiwa kutoka Kituo cha polisi cha Likoni amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Rama Ali Bamama mwenye umri wa miaka 30, alikamtwa siku ya Jumatatu akiwa na wenzake wawili waliofanikiwa kutoroka.

Bunduki hiyo ya G3 yenye nambari ya usajili 77097156 inadaiwa kuibiwa kutoka kituo hicho mapema mwezi Juni.

Rama anadaiwa kutekeleza visa kadhaa vya uhalifu ikiwemo wizi wa mabavu.

Mwendesha mashtaka Josphine Mwaura aliwasilisha ombi mahakamani la kutaka Rama kuzuiliwa kwa muda wa siku 14 ili kutoa nafasi kwa polisi kukamilisha uchunguzi wao.

Hata hivyo, Hakimu mkaazi Martin Rabera aliagiza mshukiwa huyo kusalia korokoni katika Kituo cha Polisi cha Likoni kwa muda wa siku tano.