Mshukiwa huyo aliachiliwa huru kufuatia ukosefu wa ushahidi wa kutosha. [Picha/ the-star.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa anayedaiwa kumbaka mtoto wa miaka 14 na kumpachika mimba ameachiliwa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Mohammed Omar Koti anadaiwa kumbaka mtoto huyo mnamo Septemba 6, 2014 katika eneo la Shika Adabu gatuzi dogo la Likoni.

Koti aliachiliwa huru baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka mitatu tangu kukamtwa kwake.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu mkuu wa Mombasa Evance Makori alisema kuwa upande wa mashtaka ulikosa kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa DNA ili kuthibithisha iwapo mtoto aliyezaliwa ni wa Koti.

“Hakuna ushahidi wa DNA kuonyesha kama mtoto aliyezaliwa baada ya kisa cha ubakaji zinaambatana na za mshukiwa huyu,” alisema Hakimu Makori.

Aidha, hakimu huyo ameitaka afisi ya mkuregenzi mkuu wa mashtaka ya umma pamoja na maafisa wa polisi kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuwasilisha kesi zozote mahakamani, ili haki kupatikana.

“Ningependa kuwahimiza kufanya uchunguzi vizuri ili haki na usawa upatikane kwa pande zote mbili,” alisema Makori.