Mshukiwa wa kundi la al-Shabaab ameachiliwa huru na Mahakama ya Mombasa baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha wa kumhusisha na ugaidi.
Fathia Salim alitiwa mbaroni juma lililopita katika eneo la Mwembe Kuku kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kufadhili kundi la al-Shabaab.
Hii inajiri baada ya mwendesha mashtaka Lydia Kagori kuiambia mahakama kuwa uchuguzi uliofanywa hauonyeshi kuwa mshukiwa huyo ana uhusiano na kundi hilo la kigaidi.
Salim alizuiliwa korokoroni kwa siku tano baada ya kutiwa mbaroni juma lililopita.
Siku ya Ijumaa, Hakimu mkuu katika Mahakama ya Mombasa Julius Nang’ea alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi, itakuwa bora na haki kumuachilia mshukiwa huyo bila masharti.