Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Alhamisi kuwa mshtakiwa, Sidi Ramadhani, anadaiwa kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Mshtakiwa huyo alikamatwa tarehe 2 mwezi wa Aprili, katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa.

Ramadhani anakabiliwa na mashtaka ya kupatikana na DVD nane zinazodaiwa kuwa za mafunzo ya kigaidi, pamoja na kujaribu kuiba nyaya za Kampuni ya Kenya Power zenye thamani ya shilingi laki mbili.

Mshukiwa alikana mashtaka hayo mbele Hakimu Nicholas Njagi.

Hakimu Njagi aliagiza mshtakiwa huyo kuzuiliwa hadi tarehe 4 mwezi Mei, atakaporegeshwa mahakamani ili kujumuisha mashtaka yanayomkabili.