Mshukiwa wa mauaji ya mwanamitindo kutoka Mombasa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 400,000.
Mshukiwa huyo, Robert Waliaula, anadaiwa kuiba simu na kisha kumuua mwanamitindo Janet Asunah mnamo Julai 7, mwaka huu.
Waliaula alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Viola Yator siku ya Alhamisi.
"Sikuhusika katika mauaji ya Janet. Hiyo ni njama ya kuniharibia jina,” alisema mshikuwa huyo.
Bi Asunah alipatikana akiwa ameuawa mnamo Julai 7, mwaka huu, katika nyumba yake eneo la Kizingo, Kaunti ya Mombasa.
Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 3, mwaka huu.