Mshukiwa wa mauaji ya mwanamitindo Janet Asunah atazuiliwa rumande kwa muda wa siku nane ili kutoa nafasi kwa uchunguzi kukamilika.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya afisa wa upelelezi Dancan Amoyo kuiomba mahakama kumpa muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wa kesi inayomkabili Saidi Sharif.

"Naomba muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wangu, ndio nimfungulie mashtaka mshukiwa huyo,” alisema Amoyo.

Ombi hilo liliwasilishwa mbele ya Hakimu Lilian Lewa aliyekubali ombi hilo la kumzuia mshukiwa huyo rumande.

Siku ya Jumanne, maafisa wa usalama walimtia mbaroni mshukiwa Said Sharif, akiwa katika eneo la Mwembe Tayari akiuza simu aina ya Infinix iliyokuwa ya mwendazake mwanamitindo Janet Asunah.

Bi Asunah alipatikana akiwa ameuawa mnamo Julai 7, mwaka huu, katika nyumba yake eneo la Kizingo, Kaunti ya Mombasa.

Kufikia sasa washukiwa wanne wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji ya mwanamitindo huyo.