Mshukiwa wa mauaji ya watu 12 katika eneo la Hindi Kibokoni, Swalehe Auni, alitokwa na machozi alipokuwa akielezea Mahakama kuu jinsi alivyopigwa sehemu za siri na maafisa wa KDF.
Mshukiwa aliambia Mahakama kuu ya Mombasa siku ya Alhamisi kuwa alipelekwa msituni na wanajeshi na kupigwa sehemu zake za siri, huku akilazimishwa kukubali kuhusika na mauaji hayo.
Aliongeza kuwa wenzake wawili walipigwa risasi hadi kufariki na wanajeshi hao.
Aidha, alishikilia msimamo wake mbele ya Jaji Martin Muya kuwa hakuhusika na mauaji hao wala kuenda Somalia na kujiunga na kundi la wanamgambo wa al-Shabab kama inavyodaiwa na maafisa hao.
Auni aliaimbia mahakama kuwa hana chuki wa uhasama na jamii ya Wakikuyu kama inavodaiwa, ikizingaitiwa alioa bibi wa jamii hiyo, na kuzaa naye watoto wawili.
Wiki iliyopita, Jaji Martin Muya aliwapata na kesi ya kujibu kuhusiana na mauaji hayo ya mwaka 2014 huko Lamu.
Swaleh Shebe na Joseph Kimani wanadaiwa kuhusika katika mauaji ya watu 12 katika eneo la Hindi, Kaunti ya Lamu, kati ya Julai 5 na 6 mwaka 2014.