Mahakama kuu jijini Mombasa imemuhukumu kifo mshukiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la waislamu, CIPK, marehemu sheikh Mohamed Idris.

Share news tips with us here at Hivisasa

,Mnamo Juni 10 ,2014, Mohamed Soud, anadaiwa kuhusika katika mauwaji ya marehemu Sheikh Mohamed Idris katika eneo la Likoni.

Siku ya Ijumaa, jaji Martin Muya alisema kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka unaonyesha wazi kuwa mshukiwa ndie aliyehusika pakubwa katika kumpiga risasi hadi kufariki sheikh Idris.

Mshukiwa yuko na siku 14 za kukata rufaa.

Mwezi Disemba mwaka jana, Soud, aliwalaumu maafisa wa usalama kwa kumhusisha na mauwaji hayo, umiliki wa bunduki na kilipuzi, ikizingatiwa hana ujuzi wa kutumia silaha hizo hata kidogo.