ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika mahakama ya Mombasa kwa madai ya ubakaji.
Mshukiwa huyo, Sudi Juma, anadaiwa kumbaka msichana wa umri wa miaka 13 mnamo tarehe 31 mwezi wa Octoba, mwaka wa 2015, katika eneo la Likoni.
Juma alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Irene Ruguru siku ya Jumanne.
Hakimu Ruguru aliagiza mshukiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 16 mwezi wa Mei.