Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kumbaka mototo wa miaka kumi.
Upande wa mashtaka ulieleza mahakama siku ya Ijumaa kuwa mshtakiwa, Omar Mohamed, anadaiwa kumbaka mtoto huyo katika eneo la Sheli Beach huko Likoni mnamo Novemba 5, 2015.
Omari alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache na kuitaka mahakama kumuachilia kwa dhamana.
“Sikuhusika kabisa katika ubakaji wa mtoto huyo. Hizo ni dhana tu nasingiziwa na naomba mahakama iniachilie kwa dhamana,” alisema Omar.
Hakimu Mochache alikubali ombi hilo na kumtoza dhamana ya Sh200,000.
Kesi hiyo itasikizwa Januari 7, 2016.