Mwanamume mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la ubakaji.
ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Mshtakiwa huyo, Dominic Mutua, anadaiwa kumbaka mtoto wa umri wa miaka mitano, mwezi wa nne katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa.
Mshukiwa huyo alikana shtaka hilo siku ya Jumatano mbele ya Hakimu Susan Shitubi.
Hakimu Shitub aliagiza mshukiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano.
Kesi hiyo itasikizwa mwezi Aprili tarehe 27.