Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Picha/ the-star.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama kuu ya Mombasa imedinda kumuachilia huru mwanamume aliyefungwa maisha kwa mashtaka ya ubakaji na kumpachika mimba mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 18.Alargic Jembe anadaiwa kumbaka na kumpachika mimba msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 kati ya Januari na Septemba mwaka 2014 katika eneo la Kisauni.Jembe alikata rufaa mbele ya Mahakama kuu ya Mombasa akitaka kuachiliwa huru, kwa kusema kuwa mahakama ya chini haikufanya haki na usawa katika uamuzi wake.Akitupilia mbali rufaa hiyo siku ya Ijumaa, Jaji Njoki Mwangi alisema kuwa ushahidi unaonyesha kuwa mshtakiwa alimbaka mtoto huyo.“Kulingana na ushahidi ni wazi kuwa jamaa huyu alihusika katika ubakaji wa mtoto huyu kwa hivyo mahakama haiwezi kumuachilia huru,” alisema Njoki.Jaji Njoki ameagiza mshtakiwa kuendelea na kifungo chake cha maisha kama alivyo agizwa na mahakama ya chini.