Mzee mwenye umri wa makamo atazuiliwa kwa wiki mbili gerezani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu.
Kati ya mwaka 2013 na Julai mwaka 2015, Muhammed Ahmed anadaiwa kufanya mapenzi na mtoto huyo mdogo katika eneo la Bullo Gatuzi dogo la Kisauni.
Upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa mshukiwa huyo anafaa kuchukuliwa hatua kali za kisheria, kwani ni desturi yake ya kufanya mapenzi na watoto wadogo.
Siku ya Jumanne, Muhammed alikanusha madai hayo mbele ya hakimu Diana Mochache.
“Sijawahi fanya mapenzi na mtoto huyo kamwe, hizo ni dhana to za kuniharibia jina,” alisema Muhammed.
Mshukiwa atazuiliwa korokoroni kwa wiki mbili ili kutoa nafasi kwa uchunguzi wa madai hayo kukamilika.
Kesi hiyo itaskizwa tena mnamo Julai 6 mwaka huu.