Polisi Mombasa wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja wa ugaidi katika kivuko cha feri cha Likoni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa huyo, ambaye ni raia wa Yemen, alikamatwa siku ya Alhamisi.

Akithibitisha kisa hicho, Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Maalim Mohamed, alisema kuwa mshukiwa huyo alipatikana na picha za kijeshi pamoja na paspoti ya Yemen.

Inasemekana kuwa mwanamume huyo alikuwa akilekea Somalia lakini akapotea njia na kuwauliza wananchi, ambao baadaye walipiga ripoti kwa maafisa wa polisi.

Jamaa huyo kwa sasa anahojiwa na maafisa wa polisi kutoka kitengo cha kukabili ugaidi ATPU.