Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya Maur Bwanamaka ameachiliwa huru baada ya kuzuiliwa kwa masaa kadhaa katika kizuizi cha jengo la Mahakama ya Mombasa.Kesi hiyo inawakabili raia tisa wa kigeni kutoka Pakistan na India, na watatu kutoka Kenya, wanaodaiwa kunaswa na dawa za kulevya bandarini Mombasa zenye thamani ya shilingi bilioni 1.3.Washukiwa hao wanadaiwa kupatikana na dawa aina ya heroine kati ya tarehe Julai 7 na Julai 18 mwaka 2014.Meli ya MV Darya ilizamishwa baharini na serikali mwezi Agosti 29, 2014 baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa agizo la kuchomwa kwa meli hiyo.Bwanamaka alitiwa mbaroni siku ya Jumatano, baada ya agizo la kukamatwa kwake kutolewa na mahakama siku ya Jumatatu wiki iliyopita, baada ya kukosa kuhudhuria kikao cha mahakama.Kupitia wakili wake Willis Oluga, Bwanamaka aliimbia mahakama kuwa alikuwa amehuhdhuria kikao cha kesi nyingine katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi.Bwanamaka amewasilisha barua mahakamani kuonesha kuwa aliomba ruhusa kutohudhuria kesi hiyo ya Mombasa, ili apate nafasi ya kuhudhuria kesi nyingine katika Mahakama ya Milimani.Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu mkuu katika Mahakama ya Mombasa Julius Nange’a alitupilia mbali agizo la kutiwa mbaroni kwa Bwanamwaka na kusema kuwa mshukiwa huyo hajakosa vikao vya kesi hiyo kimakusudi.“Kulingana na ratiba za kesi hii, mshukiwa hawajai kosa vikoa ya kesi hii bila sababu mwafaka," alisema Nange’a.Aidha, Nange'a alisema kuwa barua hiyo ni wa kweli na kuongeza kuwa ni wazi mshukiwa huyo alikuwa amehudhuria kikao cha kesi nyingine jijini Nairobi.“Kulingana na barua iliyowasilishwa mahakamani, ni wazi kuwa Bwanamaka alikuwa amehudhuria kesi nyingine katika mahakama kuu ya Milimani na hakukwepa kesi ya Mombasa kimakusudi," alisema Hakimu Nange’a.Wiki iliyopita, Hakimu Nange’a aliwaachia huru raia wawili wa India waliokamatwa katika meli hiyo.Praveen Nair na Vikas Balwan ni kati ya washukiwa 12 waliotiwa mbaroni wakiwa katika meli ya MV Darya iliyodaiwa kupatika na dawa hizo aina ya heroini. Hata hivyo, afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa ilikata rufaa kupinga kuachiliwa huru kwa wawili hao.Mahakama kuu kupitia Jaji Dora Chepkwonyi itatoa aumuzi wa rufaa hiyo mnamo Disemba 22, 2017.