Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kumlawiti mvulana mwenye umri wa miaka saba.
Mshtakiwa, Evans Ojwang, anadaiwa kutekeleza kitendo hicho mnamo tarehe Machi 14, katika eneo la Shelly beach, eneo bunge la Likoni.
Aidha, anakabiliwa na shtaka mbadala la kupapasa mvulana huyo sehemu zake za siri.
Ojwang alikanusha mashtaka hayo siku ya Jumanne mbele ya Hakimu Susan Shitub na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe Mei 19, 2016.