Jamma mmoja mwenye asili ya Kizungu kutoka Ubelgiji anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Central jijini Kisumu kwa madai ya kumlawiti mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 12.
Kulingana na mvulana huyo ambaye ni yatima, mshukiwa huyo kwa jina Dirk Dekeyser alimhaidi kuwa atamsaidia kuishi maishi bora bila mateso.
Mtoto huyo alidai kuwa amekuwa akiishi na mshukiwa huyo nyumbani mwake katika eneo la Riat, Kaunti ya Kisumu na amekuwa akimlawiti kwa kipindi cha majuma mawili sasa.
Akithibitisha kukamatwa kwa mshukiwa huyo, Kamanda wa Polisi wa kawaida katika Kaunti ya Kisumu Nelson Njiri, alisema kuwa kijana huyo alipelekwa katika Hospitali moja jijini Kisumu kwa matibabu.
“Tumeanzisha uchunguzi zaidi dhidi ya mshukiwa na atafikishwa Mahakamani hivi karibuni baada ya uchunguzi huo kukamilika,” alisema Kamanda Njiri.