Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshukiwa huyo, Silas Agwana, ambaye ni mlinzi, anadaiwa kuiba zaidi ya shilingi laki tisini kutoka kwa duka la mwajiri wake.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa kutekeleza wizi huo tarehe 16 mwezi wa Aprili, katika eneo la KPA.

Mwanamume huyo alikana madai hayo mbele ya Hakimu Richard Odenyo.

Hakimu Odenyo aliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 17 mwezi wa Mei.