Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumanne kuwa mshtakiwa, Rapheal Mweru, anadaiwa kuiba simu ya mkono na vifaa vya elektroniki vya thamani ya shilingi laki nne kutoka kwa duka moja mjini Mombasa.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Daniel Ogoti.

Hakimu Ogoti aliagiza Bwana Mweru kuachiliwa kwa dhamana ya shilling elfu 50.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 18 mwezi Mei.