Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la ya wizi.
ADVERTISEMENT
Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know
Mshukiwa huyo, Juma Bwire, anadaiwa kuiba gari lenye thamani ya shilingi milioni nne mnamo tarehe 7 mwezi Aprili, katika eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa.
Mshukiwa huyo alikana shtaka hilo siku ya Jumanne mbele ya Hakimu Irene Ruguru.
Hakimu huyo aliagiza Bwire kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 27 mwezi wa Mei.