Maafisa wa polisi mjini Kisii wamemtia mbaroni mwanamume mmoja wa umri wa makamo kwa madai ya kuwa mwizi kwa kuwavamia watu mjini kisii kila wakati.
Mwanamume huyo alifumaniwa siku ya Jumanne akivunja nyumba moja katika eneo la Jogoo huku maafisa wa polisi wakimtia mbaroni.
Akitibithisha kisa hicho siku ya Jumanne mjini kisii mkuu wa polisi wilayani kisii ya kati Francis Nguli alisema mshukiwa huyo alifumaniwa amevunja nyumba na tayari alikuwa ametekeleza wizi katika nyumba hiyo ambapo aliiba mtungi wa gesi.
"Mshukiwa huyo ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi na sasa hivi yuko kwa jela kakini inabainika hii si mara ya kwanza kwa mshukiwa huyo kuhusika kwa visa vya aina hiyo ,” alisema Franciss Nguli.
Nguli pia alisema kuwa Mshukiwa huyo alipokamatwa aliwapeleka maafisa wa polisi anakoishi eneo la Daraja mbili huku bidhaa vya wizi vikipatikana nyumbani mwake .
Sasa mshukiwa huyo anasubiri kufikishwa mahakamani kusomewa mashtaka yake huku uchunguzi ukiendelea dhidi ya mshukiwa huyo.