Kijana mmoja ameponea kuchomwa na wakaazi wa eneo la Jogoo baada ya kudaiwa kuwa mwizi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kijana ambaye amepigwa asubuhi ya leo na kuumizwa vibaya kwenye kichwa na miguu amefumaniwa  na mmoja wa wakaazi hao alipomtaka ajieleze anakoishi alishindwa ndipo ikawasababisha wakaazi hao kumshuku.

Kulingana na mmoja wa waliompata John Ondara alisema kuwa kijana huyo amekuwa akionekana na vijana wengine ambao si wa eneo hilo wakizurura jambo ambalo limewafanya kushuku mienendo yao na nia yao.

“Huwa wanatembea kwenye ploti za watu wakati wakaazi hao wameenda kazini na kuwaibia vitu vya nyumbani na bidhaa nyinginezo,"alielezea mkaazi huyo.

Rose Kerubo ambaye amemiliki duka kwenye sehemu hiyo amesema kuwa aliibiwa hivi juzi mtungi wa gesi akiwa shughuli zake za kuuza dukani na aliwashuku baadhi ya vijana hao ambao wameonekana mara si moja wakuranda eneo hilo.

Hata hivyo kijana huyo alinusuriwa na mmoja wa mkaazi  ambaye aliwarai wenzake kumwacha kwa vile hawakumpata na mali ya wizi.

Mshukiwa huyo alitakwa na wakazi hao kuhama mara moja kutoka eneo hilo.