Mshukiwa mmoja wa wizi aliketezwa hadi akafa na umati wa watu Ijumaa asubuhi, baada ya njama yake na wenzake watatu ya kuiba mbuzi kutibuka katika eneo la Pundamilia , Greensteds viungani mwa mji wa Nakuru.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wenzake wawili walifanikiwa kutoroka huku mwingine akiugua majeraha wakati wa tukio hilo la mapema.

Wakaazi walioongea na wanahabari baada ya kisa hicho walisema visa vya uhalifu vimeongezeka eneo hilo katika siku za hivi maajuzi huku wakitaka vyombo vya usalama kurejesha polisi washika doria katika eneo hilo

Hata hivyo washukiwa hao walikuwa tayari wameiba mbuzi wawili na walikuwa katika harakati za kuwasafirisha kuelekea mjini Nakuru kwa kutumia pikipiki walipofumaniwa na umati

Mwili wa mwendazake ulichukuliwa na polisi wa kituo cha Central na kupelekwa katika ufuo wa jimbo la Nakuru huku aliyepokea majeraha akiendelea kupokea matibabu kwenye hospitali kuu ya jimbo la Nakuru chini ya ulinzi.

Matukio hayo yamejiri wiki moja tu baada ya wakaazi wa eneo hilo kufanya mkutano wakilalamikia kudorora kwa usalama.

“Tumekuwa tukiililia serikali kuzidisha doria eneo hili kukabiliana na wahalifu, lakini hamna kitendo kinafanyika,” mkaazi mmoja alisema.