Waendeshaji bodaboda kutoka mji wa Keroka na Metamaywa Kaunti ya Nyamira walimvamia mshukiwa mmoja wa wizi wa pikipiki na kumupiga hadi akafa.
Mshukiwa huyo alikuwa anadaiwa kuwa ndiye amekuwa akihusika katika wizi wa pikipiki katika eneo la Keroka na Metamaywa jambo ambalo liliwapelekea waendeshaji pikipiki kumfuata unyo kwa unyo na kumkabili katika eneo la Chepilat.
Kulingana na mkuu wa Polisi Timothy Nduale aliyetibithisha kisa hicho, mshukiwa huyo aliuawa baada ya kupigwa na waendeshaji hao ambao walikuwa wamejawa na ghadhabu.
“Kulingana na ripoti ambazo zilitolewa na waendeshaji pikipiki walisema kuwa marehemu amekuwa akiiba pikipiki kutoka eneo la Keroka na Metamaywa kaunti ya Nyamira na wakamfumania na kumuua hii leo," alisema Nduale.
“Tumeanzisha uchunguzi kubaini ukweli halisi kuhusiana na kile ambacho kimefanyika,” aliongeza Nduale.
Ata hivyo waendeshaji hao walienda moja kwa moja hadi eneo la Ichuni eneo bunge La Nyaribari Chache na kumshambulia mshukiwa mwingine wa wizi wa pikipiki ambaye aliokolewa na wakaazi kutokana na ghadhabu yao.
Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha Kapkatet.