Mwanaume wa umri wa makamo aliuawa siku ya Jumapili na wakaazi waliokuwa na ghadhabu katika eneo la Kiptangwanyi Nakuru.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi walidai jamaa huyo ni miongoni mwa kundi la wahalifu wanaowavamia watu kwenye eneo hilo.

"iWatu walisema amekuwa miongoni mwa watu ambao wananyofoa kazi sehemu za siri. Alishambuliwa hadi kufariki," mkaazi mmoja alisema.

Inaarifiwa mshukiwa huyo alipatikana na mavazi ya mwanabodaboda mmoja aliyeuawa kwenye eneo hilo.

Mhudumu huyo wa bodaboda alikuwa pia ameuawa siku hiyo na watu ambao hawajulikani.

Chifu Kirika wa eneo hilo hata hivyo aliwatahadharisha wenyeji dhidi ya kuchukua hatua mikononi mwao.