Mshukiwa huyo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Mombasa. Picha/modernghana.com
Maafisa wa polisi jijini Mombasa wamemtia mbaroni mshukiwa anayedaiwa kuhusika katika wizi wa shilingi bilioni 13, kutoka kwa kampuni ya mwendazake Tahir Sheikh Said, al maarufu TSS.
Mshukiwa huyo, Aweys Mohamed, anadaiwa kuiba fedha hizo kwa ushirikiano na washukiwa wengine wawili ambao wamo rumande katika kituo cha polisi cha Central.Aweys anatarajiwa kufunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Mombasa.Zein Mohammed Ahmed na Zahir Gulam Hussei Khaku ambao wamo rumande wanasubiri uamuzi wa kuachiliwa kwa dhamana.Polisi wamesema kuwa uchunguzi zaidi unafanywa ili kubaini benki ambazo zilihusika katika kutekeleza kashfa hiyo.