Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Photo/ the -star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ya Mombasa imemuachilia huru mshukuwa wa wizi wa mabavu baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.Hassan Ali Baya anadiawa kujaribu kumuibia Kelvin Kwena Lunani gari lake lenye thamani ya shilingi milioni 1.6 pamoja na simu mbili, akiwa amejihami kwa bunduki na panga katika eneo la Oshwal Timbwani, eneo bunge la Kisauni mnamo Desemba 27, 2014.Akitoa uamuzi huo, Hakimu Edgar Kagoni alisema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfunga Baya gerezani.“Hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa mbele ya mahakama, hivyo basi sioni sababu ya kumhukumu mshukiwa huyu,” alisema Kagoni.Hakimu Kagoni alisema ushahidi uliotolewa unatofautiana hivyo basi hana budi ila kumuachilia huru mshukiwa huyo.“Mashahidi wa kesi hii wametofautiana katika ushahidi wao, hivyo basi ni vigumu kwa mahakama kumfunga mshukiwa huyu,” alisema Kagoni.Ameongeza kuwa polisi walikosa kufanya uchunguzi wa kutosha katika kesi hiyo.