Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru siku ya Jumanne kwa shtaka la wizi wa mabavu.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa mshtakiwa, Kiplimo Kimutai, na wengine ambao hawakuwa mahakamani, walimwibia Edwin Wafula Sh17,000 pesa taslimu, simu ya rununu aina ya Nokia na baiskeli aina ya 'Mountain bike' tarehe Oktoba 29, 2015, katika eneo la Baraka, kwenye Kaunti ya Nakuru.

Aidha, upande huo wa mashtaka ulidai mshtakiwa pamoja na wenzake walitekeleza kosa hilo wakiwa wamejihami kwa bastola.

Kimutai alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkuu Doreen Mulekyo, na kuachiliwa kwa bondi ya Sh300,000 au shilingi Sh100,000 pesa taslimu.

Kesi dhidi ya mshtakiwa huyo itatajwa Novemba 7, 2015 na kusikizwa Januari 25, 2016.