Kijana wa umri wa makamo ameachiliwa kwa dhamana ya shilling laki mbili kwa kosa la wizi wa mifungo.
ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Mshtakiwa huyo, Boniface Musyoki, anadaiwa kuiba ng’ombe wawili wenye thamani ya shilingi 63,000, mali ya Abdell Hussein, mnamo Machi 23, 2016 katika eneo la Mazera.
Musyoki alikanusha madai hayo siku ya Jumatatu mbele ya hakimu katika mahakama ya Mombasa Irene Ruguru.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe Juni 6, 2016.