Mahakama ya Mombasa imemuhukumu kifungo cha miaka miwili nje ya jela msichana aliyekiri kumwekea mvulana wa Chuo cha anuwai cha Mombasa dawa ya kupoteze fahamu kabla ya kumuibia mali.
Msichana huyo, mwenye umri wa miaka 17, alimwekea mlalamishi, Kevin Gathenya, dawa aina ya nohypol, iliyomsababisha kupoteza fahamu.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumanne kuwa msichana huyo alichukua fursa hiyo kumuibia mlalamishi mali ya nyumba yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu katika eneo la Tudor, Kaunti ya Mombasa.
Wawili hao walipatana katika eneo la burudani la Bella Vista.
Mshatakiwa alitoraka baada ya kutekeleza wizi huo lakini akakamatwa tarehe 20, mwezi Machi katika eneo la Mariakani.