Mahakama ya Mombasa ilibaki kinywa wazi baada ya msichana anayedaiwa kuwa kahaba kukubali kosa la kutia dawa ya usingizi kwenye kinywaji cha mwanamume mmoja katika eneo la Tudor.

Share news tips with us here at Hivisasa

Siku ya Jumatano, Upande wa mashtaka uliamba mahakama kuwa mnamo Machi 20, 2016 katika eneo la Tudor, mshukiwa, Mary Wanjiku, alitia dawa aina ya Rohypnol kwenye kinywaji cha Kelvin Gathenya.

Aidha, upande huo wa mashtaka uliongeza kuwa dawa hiyo ilimfanya Bwana Gathenya kulala usiku mzima na kuamka saa sita za mchana siku iliyofuata.

Gathenya alipoamka aligundua kuwa vitu vyake vya nyumbani vimeibiwa jambo lililomfaya kupiga ripoti katika Kituo cha polisi cha Makupa.

Wanjiku alitiwa mbaroni katika eneo la Miritini, akiwa safarani kuelekea Nairobi.

Mshukiwa huyo alikubali kutekelza kitendo hicho pamoja na kuiba simu, kipatakilishi, begi, saa ya mkono na vitu vyengine vya nyumbani vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki moja.

Wanjiku alimumbia Hakimu Mkuu Susan Shitub kuwa wawili hao walikutana usiku katika mkahawa wa Bella Vista na kisha kuelewana kuenda kujivinjari kimapenzi katika nyumba ya mlalamisi huko Tudor.

Mahakama itatoa hukumu ya kesi hiyo mnamo Aprili 7, 2016, baada ya mshtakiwa kufanyiwa uchunguzi wa umri, kwa kuwa aliiambia mahakama kuwa yuko na miaka 17.