Msimamizi wa taasisi ya mafunzo ya Patana iliyoko eneo la Ganjoni, jijini Mombasa alifikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa siku ya Jumatano.

Share news tips with us here at Hivisasa

Phelista Wandati alitiwa mbaroni siku ya Jumanne kwa tuhuma za kuendesha chuo hicho bila kibali.

Wandati pia anakabiliwa na shtaka la pili la kufunza katika chuo hicho pasi kuidhinishwa na Wizara ya Elimu nchini.

Hata hivyo, Wandati alikanusha mashtaka hayo na kusema kuwa yeye ni katibu wa chuo hicho wala sio msimamizi wala mmiliki wa chuo hicho.

Mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya shilingi laki mbili ama shilingi laki moja pesa taslimu.

Kesi hiyo itasikizwa Oktoba 25, mwaka huu.