Wakaazi wanaofaidika na pesa za uzee almaarufu 'Inua jamii' kutoka kwa serikali ya kitaifa wameshauriwa kutotumia pesa hizo kupika pombe haramu na kuendesha biashara haramu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wito huo umetolewa baada ya kudaiwa kuwa huenda baadhi yao hawatumii pesa hizo za ufadhili kwa njia ya halali na kupelekea wengi kutosonga mbele katika jamii.

Kulingana na katibu wa maendeleo ya vijiji nchini Lydia Moriuki aliyezungumza mjini Kisii aliomba wale wanaofaidika na pesa hizo kununua mifugo kama ng’ombe, kuku miongoni mwa mengine mengi ili kujiendeleza.

“Hizi pesa ambazo wazee hupata kutoka kwa serikali ni za kufanyia jambo la usaidizi kujiendeleza katika jamii,” alisema Moriuki.

“Naomba msitumie pesa hizi kupika pombe haramu maana ni aibu wakati serikali inawasaidia halafu mnatumia pesa hizo kwa njia isiyo halali,” aliongeza Moriuki.

Wazee hao hupata Sh2,000 kila mwezi kutoka kwa serikali.