Wanabodaboda wote kutoka kaunti ya Kisii wameombwa kutotumiwa na wanasiasa ili wanasiasa hoa kijinufaisha wenyewe na kuwacha wanabobaboda hivyo bila kujali masilahi yao.
Akiongea jana katika hafla ya uzinduzi wa bendera ya kaunti ya Kisii, katika uga wa Gusii, mwenyekiti wa wanabodaboda hao, Mike Mose, aliwaomba vijana hao kuepukana na wanasiasa walio na nia ya kuwatumia kwa njia ya kujinufahisha wenyewe bila kujjali masaibu na changamoto wanazopitia wakati wanapofanya biashara zao za uchukuzi.
“Nawaomba wanabobaboda wote wa kaunti ya Kisii kutotumiwa na wanasaiasa kwa njia ya kuwapotoza. Jambo hilo linaweza kufanya mpoteze kazi zenu na bidii kwa kazi mnayoifanya,” alisema Mose.
Aidha, aliwataka wanasiasa wajue kuwa vijana hoa huwa na changamoto nyingi hasa baridi wakati wanapofanya biashara na wengi wao wameajiriwa na wamiliki wa pikipiki ambao huitaji pesa zao kila siku.
Mose alipongeza serikali ya kaunti ya Kisii kwa ushirikiano wao mwema na vijana wa bodaboda huku akisema kuwa yeye na vijana hao wataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha maendeleo yamefanywa kupitia sekta ya uchukuzi.
Alitaja sekta ya bodaboda kuwa bora katika Kaunti ya Kisii kwani hata wale wanaofanya kazi kwa ofisi ya serikali ya kaunti hutumia pikipiki ili kufika kazini mapema.
Wanabodaboda wa Kisii kwa sasa wako na ushirikiano mwema na Serikali hiyo kwa kuwa Serikali hiyo, ikiongozwa na Gavana James Ongwae, iliwasaidia vijana hao kuwa na muungano (Sacco) ambao utawasaidia vijana hao kujiendeleza kimaisha hasa kupata mikopo.