Hofu imetanda katika gereza la wanaume Nakuru baada ya visa kadhaa vya maambukizi ya kifua kiikuu kuripotiwa.
Inaarifiwa visa 16 vya maambukizi ya ugonjwa huo vimeripotiwa katika gereza hilo la wanaume Nakuru.
Msimamizi wa gereza hilo James Sawe amesema maambukizi hayo yamesababishwa na msongamano wa wafungwa.
Mkuu huyo alisema gereza hilo lina wafungwa zaidi ya 1000 licha ya kuwa linafaa kuwa na wafungwa 700 pekee.
Hata hivyo, akiongea siku ya Jumanne, afisa wa afya gerezani humo Julia Muringu alisema wamefanya hima kudhibiti hali hiyo na kwa hivyo hakuna haja ya hofu kuwepo.