Rais Uhuru Kenyatta amewasuta viongozi wa Cord kukoma kueneza siasa za chuki na kuungana na serikali yake katika kutumikia wananchi na kuleta maendeleo nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Uhuru akiwahutubia wananchi wa Nakuru eneo la Molo katika ziara yake siku ya Jumatano pia aliwaonya viongozi hao kukoma kutumia lugha yenye matusi kutafuta kura kwa wananchi akisema kuwa wawe na subira hadi wakati wao wa kuchukua uongozi utakapofika.

"Hakuna haja ya kuvuruga wananchi na kueneza uvumi na matasu ili uwe kiongozi,ongea polepole na kwa utulivu kwa sababu kura siyo yako ila kwa wananchi ambao wataamu wakati ukifika. Ndiyo maana nawaelezea wale wapinzani kuwa wasubiri hadi mwaka 2032 ili kuongoza nchi hii," Uhuru alisema.

Rais pia alihakikishia wakaazi wa eneo hilo kuwa serikali itaendelea kutumikia wananchi kwa ujumla bila ubaguzi ili kutimiza ahadi yao walizotoa.

"Serikali yangu itaendelea kuhakikisha kila eneo humu nchini inapata kuendelea licha ya upinzani kutoka kwa baadhi ya viongozi humu nchini. Ninawaomba viongozi hao kutupa nafasi tufanye kazi yetu ili wananchi wapate kunufaika zaidi," aliongezea.