Wachanganuzi wa maswala yanayohusiana na ugatuzi, wameonya kuwa hatua zilizoafikiwa kuimarisha sekta ya afya, huenda zikalemazwa ikiwa mswada unaohusiana na afya (Health Bill 2016) ulio utapitishwa kama ulivyo. Mswaada huo unatarajiwa kujadiliwa kwa mara ya pili sasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mtaalamu mmoja Dkt Mutakha Kangu amesema kuwa huenda mizozo iliyopo baina ya wabunge na maseneta kuhusu ubabe wa mamlaka, zimechangia pakubwa kuharakishwa kwa mswada huo.

Kangu amesema ni kinyume na matakwa ya ugatuzi kwa serikali kuu kuchukua usimamizi wa hospitali za Level 5 na Level 6 na kuzigeuza hadi kuwa hospitali za Rufaa, baada tu ya kuimarishwa kwa huduma kwenye hospitali hizo na magavana.

“Sekta ya afya ambayo imegatuliwa haihitaji utatuzi wa kisiasa. Kwa hivyo mizozo iliyopo kati ya seneti na bunge la kitaifa, isiingizwe katika mswaada huo. Serikali kuu iachie serikali za kaunti huduma za hospitali zote za level 5 na level 6,” alisema bwana Kangu kwenye siku ya pili ya warsha kuhusu afya kati ya washikadau na kamati ya seneti ya afya mjini Naivasha.

Dkt Mutakha alisema mswaada huo haujaweka mikakati dhabiti kuhusu jinsi wahudumu wa sekta ya afya watakuwa wakiajiriwa au hata kupandishwa vyeo, akisema unafaa kufanyiwa marekebisho kabla ya kupitishwa.