Mbunge wa Molo Jacob Macharia amehoji kuwa kupasishwa Kwa mswada wa jinsia kutasababisha ushuru kupanda.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza Jumatatu katika eneo bunge lake la Molo, Macharia ambaye alichaguliwa Kwa chama cha TNA alisema kuwa kupasishwa kwa mswada huo kutafanya idadi ya wabunge kuongezeka hadi 400.

"Mswada huu ukipasishwa,idadi ya wabunge itaongezeka hadi 400 na watahitaji mshahara hivyo basi sharti ushuru uongezeke,"alisema Macharia.

Alisema kuwa kunahitaji mashauriano ya mswada huo.

Macharia alitoa wito kwa wananchi katika kaunti ya Nakuru na taifa kwa jumla kuwa watulivu wakati swala hilo likishughulikiwa.

 Matamshi yake yalijiri siku moja tu baada ya viongozi mbalimbali wa jinsia ya kike kuwalaumu wenzao wa kiume waliopinga mswada huo wiki Jana.