Mswada wa sheria kuhusu thuluthi mbili ya uwakilishi wa jinsia umekosa kuungwa mkono kwa mara ya pili baada ya kuwasilishwa bungeni Alhamisi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya wabunge 178 kuupigia kura huku 16 wakiupinga nao wabunge 5 waliokuwa bungeni wakikosa kupiga kura.

Mswada huo ulihitaji kura 233 ili uweze kupitishwa

Mswada huo umekosa kupitishwa kwa mara ya pili licha ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwaomba wabunge kuunga mkono mswada huo.

Wiki jana, mswada huo ulikosa kupitishwa baada ya wabunge 195 kuunga mkono ambapo 28 waliupinga huku wabunge wengine 24 wakidinda kupiga kura.

Izingatiwe kuwa Mbunge wa Bahari Kimani Ngunjiri na Mbunge wa Njoro Joseph Kiuna kwenye mahojiano na mwandishi huyu walikariri kuwa waliupinga mswada huo ulipowasilishwa bungeni wiki jana.

Aidha, walisema wataupinga mswada huo Alhamisi hii wakisema iwapo mswaada utapitishwa utaongezea idadi ya wabunge kuwa 450, hali waliyosema ni mzigo mzito kwa mlipa ushuru hapa nchini.

Hatua hiyo ni pigo kwa wanawake miogoni mwao akiwa Spika wa bunge la kaunti ya Nakuru Susan Kihika aliyetumai kuwa bunge litapitisha mswada huo